JOHANNESBERG:Kansela Merkel akutana na Mandela | Habari za Ulimwengu | DW | 07.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JOHANNESBERG:Kansela Merkel akutana na Mandela

Kansela Angela Merkel bado anaendelea na ziara yake barani Afrika jana alikutana na rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela mjini Johannesberg.Merkel amesema mkutano wake wa dakika 45 na mzee Mandela ulimgusa.Akiwa nchini Afrika Kusini pia alizungumzia suala la mabadiliko ya hali ya hewa akisema Afrika iko hatarini zaidi kwasababu tayari imeanza kukabiliwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Aidha Kansela Merkel alitumia ziara yake hiyo kumtolea mwito rais Thabo Mbeki kumshawishi mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe kukomesha ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya raia wa Zimbabwe.

Kansela Angela Merkel leo hii ataelekea Liberia ambako amepangiwa kukutana na viongozi wa nchi hiyo baadae hii leo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com