1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Joachim Sauer mume wa kansela Merkel

Sekione Kitojo
14 Septemba 2017

Unaweza kumuelezea kansela  wa Ujerumani  Angela Merkel kama mtu mtulivu sana na huwezi kumjua sana  kile  anachofikiria kwa kumtazama  tu. Bila shaka na mume wake yuko hivyo hivyo Joachim Sauer.

https://p.dw.com/p/2juOP
Deutschland Auftakt der berühmten Richard-Wagner-Festspiele in Bayreuth
Picha: picture alliance/dpa/T. Hase

Ni mara chache ameonekan, huyo ndio Merkel na hata mume wake Joachim Sauer yuko karibu hivyo hivyo si mtu wakujitokeza mara  nyingi mbele za  watu.a pamoja  na  mkewe Merkel  katika  tamasha  la  muziki wa Opera mjini Bayreuth. Kuhusu masuala  ya  kisiasa  hasemi  lolote.

Kujitokeza  mbele  ya vyombo  vya  habari , kama  wanavyofanya baadhi  ya wake za marais wa Marekani, hilo kwa Joachim Sauer halipo kabisa. Na hata ukimlinganisha na mwenza wa kansela wa zamani Doris Schoeder-Kopf ama Hannelore Kohl, Sauer ni tofauti  kabisa. Mahojiano na  waandishi  wa habari hayapendelei kabisa. Sio kwamba ni mwenye haya, la hasha, hapendelei tu kumfunika mke wake Angela Merkel. Kama hil  halitoshi, mtu huyo  ambaye ni sehemu ya Kansela wa Ujerumani ni mtaalamu mkubwa wa masuala ya kemia, ambaye amekwisha pewa tuzo kadhaa.

Deutschland Joachim Sauer
Mume wa Kansela Angela Merkel, Joachim SauerPicha: Getty Images/AFP/T. Hanai

Profesa Dr. Sauer alianza kufanyakazi zake mwaka 1967 akifanya utafiti wa kemia katika chuo kikuu cha mjini Berlin cha Humboldt. Katika iliyokuwa Ujerumani mashariki DDR, alikuwa mmoja kati ya wanasayansi wanaoaminiwa kimataifa, ambao hawakuwa wanajihusisha na kitengo cha ujasusi cha Ujerumani mashariki. Baada ya kufanyakazi katika sehemu mbali mbali anaongoza tena leo hii kikundi cha utafiti wa kemia ya vyakula katika chuo kikuu cha Humboldt , kikifanya utafiti juu ya tathmini ya  vyakula mbali mbali na utafiti wa kinadharia kuhusu maumbo, nishati na mchakato wa mwili kuweza kuchakachua chakula.

Tuzo ya Nobel

Bayreuther Festspiele 2015 - Eröffnung Angela Merkel
Merkel akiwa na mume wake Joachim SauerPicha: picture-alliance/dpa/T. Hase

Kama uvumi uliotokea mwaka 2015, kwamba kuhusiana na hatua za Angela Merkel kufungua mipango ya nchi hii kwa  wakimbizi na wahamiaji, kumekuwa na matamshi katika duru za wataalamu, kwamba mume wake Joachim Sauer anaweza  kupata  tuzo ya Nobel ya kemia. Barack Obama alimuita wakati walipokutana na Merkel kwa kiasi kikubwa kwa jina la Profesa tu.

Sauer alimfahamu Merkel katika miaka ya 1980 wakati  wakiwa katika chuo cha sayansi mjini  Berlin. Walioana  mwaka 1989, ikiwa  wote ni ndoa ya pili. Katika ndo ya kwanza Sauer ana watoto  wawili wa kiume. Kwa upande wa Joachim Sauer kama mtu wa  kawaida hilo halijulikani. Kwa upande wa mume wake kile anachosema Merkel, ni kwamba hawazungumzi sana kuhusu siasa, lakini  pia ni mshauri mzuri kwa upande mwingine. Wawili hao wanaunganishwa na mapenzi makubwa ya muziki wa Opera na uasili, kwa  miaka kadhaa wamekuwa wakifanya safari katika majira ya joto kwenda Tirol ya kusini kutembea.

Mwandishi: Ines Eisele / ZR /  Sekione  Kitojo

Mhariri: Iddi Ssessanga