1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jimbo la Kosovo kujitangazia uhuru wake Jumapili

16 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D8aB

PRISTINA:

Jimbo la kusini la Serbia,Kosovo litajitangazia uhuru wake siku ya Jumapili.Waziri Mkuu wa Kosovo,Hashim Thaci amethibitisha kuwa jimbo hilo litajitangazia uhuru wake kutoka Serbia.Hatua hiyo inapingwa vikali na Serbia na mshirika wake mkubwa Urusi.Serbia imesema,haitotambua taifa huru la Kosovo na imetishia kuchukua hatua za kiuchumi na kidiplomasia dhidi ya madola yatakayotambua taifa huru la Kosovo.

Marekani na baadhi kubwa ya nchi za Umoja wa Ulaya,ikiwa ni pamoja na Ujerumani,zimeashiria kuwa zitaitambua nchi hiyo mpya.Mjini Brussels pia Umoja wa Ulaya umeidhinisha mpango wa kupeleka Kosovo ujumbe wa kama maafisa 1,800 kuisaidia Kosovo kujenga taifa lenye utawala wa kisheria.Ujumbe huo utakuwa na polisi,wataalamu wa sheria pamoja na usimamizi.