Jifunze Kijerumani kwa ″Podcast″ | Podcasting & Feeds | DW | 18.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Podcasting & Feeds

Jifunze Kijerumani kwa "Podcast"

Jifunze Kijerumani kwa Podcast kutoka DW. Kutoka Kijerumani cha kila siku, taarifa za habari zinazosomwa polepole hadi mafunzo kamiili ya lugha, hamishia kwenye kompyuta (tarakilishi) yako na uanze kujifunza!

Jifunze Kijerumani kupitia DW-WORLD.DE: Wakati wowote, mahali popote!

Jifunze Kijerumani kupitia DW-WORLD.DE: Wakati wowote, mahali popote!

Neno "Podcasting" linatokana na "iPod," MP3 player ya Apple, na "broadcasting" yaani utangazaji. Kimsingi "podcasts" ni sawa na redio kwenye iPod yako. Ni lazima mtu ajisajili kutumia "Podcasts" na zinapatikana mara moja pindi ziwapo tayari. Jisajili kupitia wavuti wa DW au iTunes Music Store.

Zinapatikana daima, hazigharimu chochote.

Ukiwa na "Podcasts", unaweza kupata vipindi vingi vya DW vya kusikiliza au kutazama wakati wowote. Unaweza kuratibu vielelezo vyako vya sauti au video kwenye MP3 Player yako. Huhitaji iPod pekee kupata "podcasts"; MP3 Player yoyote inafaa. Inakutegemea wewe mwenyewe, wakati, mahali na jinsi unavyotaka kusikiliza sauti ulizochagua. Shughuli hii ni rahisi zaidi hasa ukizingatia kuwa podcasts za DW hazikugharimu chochote.

Jinsi inavyofanya kazi

Ili kujisajili kwenye podcast unahitaji kompyuta (tarakilishi) iliyounganishwa na mtandao wa tovuti pamoja na kiungo cha sauti kama vile iTunes. Kwa jinsi hii unaweza kujisajili kupata vipindi vyako bora vya DW na kuvihamishia kwenye kompyuta (tarakilishi) yako au MP3 player. Kila unapofungua kielelezo chako cha sauti, kinachunguza "podcast" zako na kuhamisha mara moja viungo vipya.

Baada ya kujisajili kwenye podcast na ikahamishwa kwenye kompyuta yako, unachohitaji ni kuhamishia kiungo cha sauti kwenye MP3 player yako. Mhimili mkuu wa "podcasts" ni iPodder pamoja na viungo kama vile iTunes (angalia kiungo kilicho chini) na vyote hivyo vinapatikana bila malipo kwenye tovuti.

Uteuzi mpevu

DW ndilo shirika la kwanza la umma la utangazaji (habari) kutoa huduma ya podcast lilipowapa wasikilizaji wake vipindi vya uchaguzi wa urais wa mwaka 2004. Mpango huo ulioanza kwa vipindi vya sauti pekee ulipanuliwa kujumuisha kanda za video kutoka runinga ya DW-TV. Leo hii DW-WORLD.DE inatoa huduma ya "podcast" tofauti zaidi ya hamsini ambazo ni vipindi vya redio na runinga (televisheni), masomo ya Kijerumani na makala maalumu kutoka maktaba ya Deutsche Welle.

DW inapendekeza