Jeshi la Niger lalaumiwa kwa raia 102 kupotea | NRS-Import | DW | 05.09.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

NRS-Import

Jeshi la Niger lalaumiwa kwa raia 102 kupotea

Jeshi la Niger limehusika na kupotea kwa watu zaidi ya watu 100 katika eneo la magharibi la nchi hiyo.

Shirika hilo lilitumia miezi kadhaa likichunguza kupotea kwa raia katika ukanda wa Inates eneo la Tillaberi. Kundi hilo lilichapisha ripoti yake siku ya Ijumaa.

"Kilichotokea Inates hakitakiwi kutokea tena" alisema katibu mkuu wa shirika hilo, Ali China Kourgueni. "Kazi iliyobaki sasa ni kwa mamlaka ya mahakama," aliongeza kusema.

Serikali imepokea ripoti hiyo, lakini haijatoa kauli yoyote.

Upoteaji wa watu hao ulitokea baada ya shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa kiislamu katika kituo cha kijeshi huko Inates mnamo mwezi Desemba ambapo wanajeshi wapatao 71 waliuliwa.

"Sio suala la kulitia hatiani jeshi lote la Niger, ni suala la kuwatambua baadhi ya wanajeshi wasiodhibitika wanaotakiwa kulaumiwa kwa mauaji hayo na upoteaji wa raia 102 katika eneo la Tillaberi," alisema Kourgueni.

Wanajeshi nchini Niger na mataifa jirani ya Mali na Burkina Faso wamelaumiwa kwa ongezeko la idadi ya mauaji ya watu kinyume na sheria na ukiukaji mwingine huku wakipambana na ongezeko la uasi katika eneo la mpaka wa mataifa hayo matatu.

(afp)