1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Marekani imepeleka vikosi kunusuru maafisa wake Haiti

Sudi Mnette
11 Machi 2024

Jeshi la Marekani limesema limepeleka vikosi kadhaa kwa ndege chini Haiti kwa kile ilichokieleza kuongeza ulinzi katika ofisi za ubalozi wake na kutoa nafasi ya maafisia pia kuondoka nchini humo kwa usalama.

https://p.dw.com/p/4dMr3
Haiti Port au Prince | Vurugu za magenge
Vikosi vya Kitengo cha Usalama Mkuu wa Ikulu ya Kitaifa, USGPN, waliweka ulinzi huko Port-au-Prince, Haiti, Jumamosi, Machi 9. , 2024.Picha: Odelyn Joseph/AP/picture alliance

Hatua hiyo inatoa picha ya hofu ya mashaka maafisa waandamizi wa serikali ya Haiti kwamba wanaweza kuikimbia nchi hiyo katika kipindi hiki ambacho mashambulizi yanaongezeka.

Maeneo ya karibu na ubalozi katika mji mkuu, Port-au-Prince, kwa kiasi kikubwa inadhibitiwa na magenge ya waovu.

Taarifa hiyo ilielezea hali ya usalama nchiniHaiti kuwa dhahiri isiyo madhubuti na kuongeza kuwa inasababisha tishio la moja kwa moja kwa usalama na utulivu wa taifa.