1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la jamhuri ya kidemokrasi ya Congo lakabiliwa na matatizo ya kinidhamu.

Sekione Kitojo23 Juni 2009

Matatizo ya kinidhamu, ucheleweshaji wa mishahara na matatizo ya usafirishaji ni baadhi ya mambo yanayolikabili jeshi la Congo.

https://p.dw.com/p/IXkb


Ucheleweshaji wa malipo ya mishahara, nidhamu na matatizo ya usafirishaji na ugavi wa mahitaji vinatishia uwezo wa jeshi kuweza kuwashinda waasi kutoka Rwanda na Burundi na kuleta amani katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Bado hali ni mbaya, kwa mujibu wa gazeti la mjini Kinshasa la Le Potentiel, likielezea kutokuwepo na uwezo kwa jeshi la serikali ya jamhuri ya kidemokrasi ya Congo kumaliza ghasia na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya raia katika jimbo la Orientale na Kivu ya kaskazini na kusini.

Majeshi hayo ambayo yana karibu wanajeshi 140,000, yakisaidiwa na wanajeshi 17,000 wa umoja wa mataifa wa kulinda amani, wameshindwa kulishinda jeshi wa waasi wa Kihutu kutoka Rwanda lenye wanajeshi wapatao 5,000 hadi 6,000 na kati ya wapiganaji kutoka Uganda wanaofikia kiasi cha 400 hadi 500 katika misitu na milima ya mashariki ya jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Uharakishaji wa kuwaingiza katika jeshi hilo waasi wa zamani maelfu kadha wa kundi la national Congress for the Defence of the People CNDP kulilenga kuimarisha mkono wa jeshi hilo la Congo, lakini badala yake hatua hiyo imelidhoofisha wamesema wadadisi.

Jeshi la Congo , FARDC linapitia kipindi kigumu cha mpito, kuwaingiza waasi wa zamani katika jeshi hilo kunasababisha matatizo katika ngazi zote.

Kulifanya kuwa jeshi lenye uwezo wa mapambano kutoka katika kundi hili ni changamoto kubwa, amesema Kevin S.Kennedy, mkurugenzi wa habari katika umoja wa mataifa mjini Kinshasa.

Hatua hiyo imekumbwa na matatizo kadha tangu kuanzishwa mapema mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kucheleweshwa kwa hatua za kupata idadi ya wanajeshi wote wapya, kwa msingi kwamba kima cha chini cha mshahara cha dola 64 kwa mwezi kimekuwapo kwa muda wa miezi kadha sasa.

Hali hiyo imesababisha wanajeshi kuliacha jeshi, uasi na upinzani. Vikosi vimekataa hata kwenda katika baadhi ya operesheni. Matukio kama haya yameongezeka hivi karibuni, zimesema duru za kijeshi kutoka mataifa ya magharibi.

Katikati ya Juni mwaka huu wanajeshi 27 ambao walikuwa hawajalipwa walifyatua risasi dhidi ya kituo cha kijeshi cha umoja wa mataifa huko Kivu ya kaskazini kabla ya kukamatwa.

Usafirishaji wa mahitaji haujakuwa mzuri ama mahitaji hayo huuzwa kwa mfano katika chakula na mafuta. Silaha, na madawa havifiki kwa wahusika pia, kimesema chanzo kimoja.

Morali umeshuka kwasababu ya matatizo haya, lakini pia kwasababu baadhi yao wamekuwa katika mapambano kwa muda wa miaka kadha, bila ya kupumzishwa. Wanajeshi wanaishi katika vituo vyao na familia zao, na umuhimu mkubwa uliopo ni kuwalinda, ama kukimbia kutoka makambi hayo.

Amesema kuwa operesheni ya kijeshi upande wa mashariki ilitabiriwa kushindwa.

Katika hatua kama hiyo operesheni ya hivi sasa ya kijeshi dhidi ya waasi inaweza kushindwa, kwa mujibu wa Guillaume Lacaille, wa kundi la kimataifa linaloshughulikia mizozo, akisema kuwa mkakati mpya unahitajika kwa ajili ya majeshi ya Congo.

Jibu linaweza kuwa liko katika kuunda vikosi vidogo ili kuvunja uhusiano kati ya wapiganaji wa kundi la Kihutu kutoka Rwanda la FDLR pamoja na viongozi wao wenye msimamo mkali, ikiwa inafahamika wazi kuwa baadhi yao walishiriki katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.




Mwandishi : Sekione Kitojo /IPS

Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman