1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Iran latishia kushambulia vikosi vya Marekani

4 Mei 2026

Jeshi la Iran limeionya Marekani kwamba itavishambulia vikosi vyake ikiwa vitasaidia meli zilizokwama kupita kwenye Mlango Bahari wa Hormuz .

https://p.dw.com/p/5DDZc
Oman Musandam 2026 | Hormuz
Boti katika Mlango-Bahari wa Hormuz mnamo Aprili 29, 2026Picha: REUTERS

Meja Jenerali Ali Abdollahi wa kamandi kuu ya jeshi la Iran ametoa onyo hilo dhidi ya vikosi vyovyote vya kigeni na haswa Marekani.

Abdollahi ameongeza kusema usalama wa Mlango-Bahari wa Hormuz unadhibitiwa na vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na katika mazingira yoyote, njia yoyote salama lazima iratibiwe na vikosi vya jeshi hilo.

Wakati huo huo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amepongeza tangazo hilo la msaada kutoka kwa Trumo lakini akafutilia mbali uwezekano wa ushiriki wa Ufaransa katika zoezi hilo.