1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGuinea-Bissau

Jeshi la Guinea-Bissau lawaachia wanasiasa 6 wa upinzani

24 Desemba 2025

Utawala mpya wa kijeshi nchini Guinea-Bissau umetangaza kuwa umewaachia huru wanachama 6 wa chama kikuu cha upinzani waliowakamata na kuwazuia korokoroni tangu yalipotokea mapinduzi ya kijeshi mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/55ugX
Guinea-Bissau Bissau 2025 | Baraza Tawala la Kijeshi nchini Guinea-Bissau
Baraza Tawala la Kijeshi nchini Guinea-Bissau.Picha: Patrick Meinhardt/AFP

Wanachama hao sita walioachiwa walikuwa na mafungamano na Domingos Simoes Pereira, ambaye ni mkuu chama cha siasa cha PAIGC kilichoiongoza nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1974. Pereira mwenyewe bado yuko kizuizini tangu jeshi lilipofanya mapinduzi.

Baraza Tawala la Kijeshi la nchi hiyo limesema kuachiwa kwa wanasiasa hao 6 ni "ishara ya nia njema kuelekea kurejea kwa utawala wa kikatiba na kuheshimiwa kwa haki za binadamu".

Jeshi la Guinea Bissau lilichukua madaraka kwa njia ya mapinduzi mnamo Novemba 26 na kuuangusha utawala wa Rais Umaro Sissoco Embalo ambaye hivi sasa amekimbilia uhamishoni.