Jerusalem.Wanadiplomasia wa Ujerumani washambuliwa.
30 Desemba 2006Matangazo
Jeshi la Israel limesema kuwa wapiganaji wa Palestina wamefyatua risasi dhidi ya mlolongo wa magari ya wanadiplomasia wa Ujerumani. Hakuna ripoti za watu walioumia.
Mashambulizi hayo yalitokea karibu na Ramallah. Wanajeshi wa Israel baadaye walipekua eneo hilo lakini hawakupata mtuhumiwa yeyote.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani imekataa kusema lolote kutokana na sababu za kiusalama.