1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem:Olmert aondoa matumaini ya haraka katika mkutano wa mashariki ya kati.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Dm

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema mkutano wa mashariki ya kati utakaodhaminiwa na Marekani na unaotarajiwa mwezi ujao, haukusudii kuwa tukio la aina yake au kuleta makubaliano yoyote ya kihistoria. Akizungumza kabla ya kuelekea Ufaransa na Uingereza leo, hata hivyo waziri mkuu huyo wa Israel alisema mkutano unaopangwa huko Annapolis-Maryland-Marekani, uangaliwe kuwa ni nafasi kwa jamii ya kimataifa kuunga mkono majadiliano juu ya dola ya Palestina yanayotarajiwa kuanza baada ya mkutano huo.Wajumbe wawili wa mrengo wa kulia katika serikali ya muungano ya Bw Olmert wametishia kujitoa ikiwa mkutano huo utayatatua masuala muhimu ikiwa ni pamoja hatima ya mji wa Jerusalem na maeneo yake matakatifu.