1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM.jeshi la Israel laanzisha uchunguzi kuhusu mabomu ya mtawanyiko

20 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqz

Jeshi la Israel limeanzisha uchunguzi kuhusu matumizi ya mabomu ya mtawanyiko bila ya amri wakati wa vita vya Lebanon.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka duru za kijeshi za Israel mkuu wa majeshi wa Israel Luteni jenerali Dan Halutz amekataza matumizi wa mabomu hayo.

Uchunguzi wa kijeshi ulionyesha kwamba jeshi la Israel lilitumia mabomu ya mtawanyiko wakati wa vita vya na Lebanon.

Shairika la kutetea haki za binadamu pia limelaani utumizi wa mabomu hayo dhidi ya makaazi ya binadamu wakati wa vita hivyo.

Zaidi ya watu 20 waliuwawa katika mashambulio ya mabomu ya mtawanyiko na takriban watu 70 walijeruhiwa.