JERUSALEM:Ehud Olmert afanya mabadiliko kidogo ya baraza lake la mawaziri | Habari za Ulimwengu | DW | 04.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM:Ehud Olmert afanya mabadiliko kidogo ya baraza lake la mawaziri

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amefanya mabadilko katika baraza lake la mawaziri leo hii ili kujaza nafasi zilizoachwa na baadhi ya mawaziri waliojiuzulu kufuatia kashfa mbali mbali.

Ronnie Bar-On ambaye ni msiri wa muda mrefu wa Ehud Olmert ametangazwa kuwa waziri wa fedha akichukua mahala pa Avraham Hirchson aliyejiuzulu jumapili kufuatia uchunguzi wa polisi juu ya madai ya kuhusishwa na ubadhirifu wa mali katika chama cha wafanyikazi alichokuwa akikisimamia mwaka 2003.Kujiuzulu huko kwa Hichson lilikuwa ni pigo kubwa kwa waziri mkuu Olmert ambaye alikuwa akimtambua kama smhirika wake mkuu katika chma cha Kadima.Haim Ramon naye ndie naibu waziri mkuu akichukua mahala pa Shimon Peres ambaye amechaguliwa hivi karibuni kuwa rais wa taifa hilo la Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com