JERUSALEM : Wanamgambo wafyatuwa roketi dhidi ya Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 14.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM : Wanamgambo wafyatuwa roketi dhidi ya Israel

Jeshi la Israel limesema wanamgambo wa Kipalestina wamefyetuwa roketi hadi ndani mwa Israel leo alfajiri na kukiuka usitishaji wa mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Roketi hilo limeangukia kwenye mji wa Nir Am karibu na mpaka na Gaza lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.Maafisa wa jeshi wa Israel wanasema wanamgambo wa Kipalestina wamefyetuwa zaidi ya maroketi 20 dhidi ya Israel tokea kuanza kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na wanamgambo hao wa Kiaplestina hapo tarehe 26 mwezi wa Novemba.Maroketi hayo hayakusababisha maafa lakini kumekuwepo na mfululizo wa matukio ambapo kwayo wanajeshi wa Israel waliwapiga risasi Wapalestina waliokuwa wakiosegelea mpaka wenye ulinzi mkali wa Gaza na Israel.

Hapo Jumaatano wanajeshi hao walimuuwa mwanamgambo wa kundi la Fatah mwenye umri wa miaka 22 kwenye uzio wa mpaka huo.

Hata hivyo matukio hayo hadi sasa yameshindwa kuvuruga suluhu ilioko kati ya pande hizo mbili.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com