JERUSALEM: Waisraeli wamtaka Olmert ajiuzulu | Habari za Ulimwengu | DW | 01.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Waisraeli wamtaka Olmert ajiuzulu

Waisraeli hii leo wamemshinikiza waziri mkuu Ehud Olmert ajiuzulu huku serikali yake ya mseto ikianza kusambaratika kufuatia ripoti ya vita vya Lebanon.

Ripoti hiyo iliikosoa vikali serikali ya Ehud Olmert kwa kushindwa vibaya katika vita hivyo. Waziri mmoja katika baraza la mawaziri, Eitan Cabel, amejiuzulu hii leo akisema hawezi kuendelea kubakia katika serikali inayoongozwa na waziri mkuu Ehud Olmert. Waziri huyo amesema wananchi wa Israel wamepoteza imani na waziri mkuu Ehud Olmert.

Uamuzi wake umeongeza mbinyo dhidi ya Ehud Olmert ambaye anazidi kukabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa chama chake cha Kadima ajiuzulu.

Vyombo vya habari nchini Israel vimemnukulu mwanachama wa chama cha Kadima akisema ripoti hiyo huenda ikapendekeza waziri mkuu Ehud Olmert pamoja na waziri wake wa ulinzi, Amir Perez, wajiuzulu.

Olmert mwenyewe amesema hatajiuzulu kufuatia ripoti hiyo lakini anachukua dhamana kwa kushindwa kuyatimiza malengo ya vita vya Lebanon.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com