1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Waisrael na Wapalestina washindwa kuafikiana katika mazungumzo.

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJy

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa Palestina Mahmoud Abbas wamekutana kwa mazungumzo mjini Jerusalem. Maafisa kutoka pande zote mbili wamesema hakuna hatua za maendeleo zilizofikiwa katika masuala muhimu wakati wa mkutano huo wa saa mbili.

Hata hivyo , viongozi hao wawili wamekubaliana kuendelea na mazungumzo yao.

Mkutano huo unakuja kabla ya kutangazwa kwa serikali mpya ya umoja wa kitaifa ya Palestina itakayotangazwa na waziri mkuu Ismail Haniyeh wa chama cha Hamas. Olmert amesema kuwa Israel itasusia serikali hiyo ya umoja wa kitaifa ambayo inaundwa kati ya chama cha Abbas na chama cha Hamas hadi pale itakapoitambua Israel, kukana matumizi ya nguvu na kukubali makubaliano yaliyokwisha fikiwa ya amani. Madai hayo yameidhinishwa pia na kundi linaloshughulikia mzozo huo wa mashariki ya kati kundi linalojumuisha Marekani, umoja wa Ulaya, umoja wa mataifa na Russia. Hapo mapema , mpiganaji mmoja wa Kipalestina aliuwawa katika mapambano mapya kati ya makundi hasimu ya Hamas na Fatah katika ukanda wa Gaza.