1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Viongozi wa Hamas huenda wakalengwa na Israel

22 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzU

Israel imesema,Waziri Mkuu wa Wapalestina,Ismail Haniyeh wa chama cha Hamas,huenda akalengwa katika mashambulio ya siku zijazo.Naibu waziri wa ulinzi wa Israel,Ephraim Sneh amesema,makamanda na viongozi wa Hamas wanaweza kulengwa katika siku zijazo.Israel,imetamka hayo,baada ya mwanamke mmoja wa Kiisraeli kuuawa na watu wengine 2 kujeruhiwa katika mashambulio ya makombora yaliyofanywa na wanamgambo wa Kipalestina dhidi ya mji wa Sderot kusini mwa Israel.Leo,ndege za kivita za Israel zilirusha makombora katikati ya Gaza.Kwa mujibu wa maafisa wa Kipalestina,watu 7 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo.