JERUSALEM: Rais Abbas akutana na waziri mkuu Ehud Olmert | Habari za Ulimwengu | DW | 28.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Rais Abbas akutana na waziri mkuu Ehud Olmert

Rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, amejtana leo na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, mjini Jerusalem.

Rais Abbas amemuonya Olmert kwamba mkutano wa mashariki ya Kati uliopendekezwa na Marekani kuhusu kuufufua mchakato wa kusaka amani huenda usiwe na maana yoyote.

Abbas amesema mkutano wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu, hautakuwa na maana kama utazingatia tu kutangaza kanuni. Ehud Olmert amemkaribisha rais Abbas kwenye ikulu yake mjini Jerusalem kwa mazungumzo yatakayohusu kuziendeleza taasisi za Palestina, kuisaidia serikali ya rais Abbas na maswala ya Waisraeli na Wapalestina wanaoishi pamoja.

Rais Abbas na Ehud Olmert walikutana mara ya mwisho mnamo tarehe 6 mwezi huu mjini Jericho, huko Ukingo wa magharibi wa mto Jordan, ambapo viongozi wa Israel na Palestina walitofautiana kuhusu maswala ya mipaka, hatima ya mji wa Jerusalem na wakimbizi wa kipalestina.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com