JERUSALEM : Olmert ahojiwa na wapelelezi | Habari za Ulimwengu | DW | 11.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM : Olmert ahojiwa na wapelelezi

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert leo amehojiwa kwa mara ya pili wiki hii kutokana ana madai ya kutumia vibaya ushawishi wake katika ubinafsishaji wa mojawapo ya benki mashuhuri nchini humo.

Uchugunzi juu ya ubinafsishaji wa Benki ya Leumi hapo mwaka 2005 ni mojawapo ya upepelezi wa jinai unaomuandama waziri mkuu huyo.Imeelezwa kuwa wapepelezi wamekuwa wakimhoji Olmert chini ya hadhari.

Polisi inatuhumu kwamba Olmert wakati huo akiwa waziri wa fedha katika serikali ya Waziri Mkuu Ariel Sharon alijaribu kushawishi uuzaji wa Benki ya Leumi ambayo ni benki ya pili kwa ukubwa nchini Israel kwa rafiki yake wa Australia Frank Lowey.

Benki hiyo hatimae imeuzwa kwa kampuni nyengine isiokuwa na uhusiano na Lowey.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com