1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Maaskofu wa Ujerumani wako Israel

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCN1

Kundi la Maaskofu wa madhehebu ya Kikatoliki wa Ujerumani limetembelea eneo la kumbukumbu ya Maangamizi ya Wayahudi la Yad Vashem nchini Israel kutowa heshima zao kwa Wayahudi waliouwawa na utawala wa Manazi wa Ujerumani.

Kadinali Karl Lehmann amesema mauajji hayo ya umma wa Mayahudi hayapaswi kusahauliwa kamwe.Maaskofu hao pia walikutana na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi.Ziara yao inakuja wakati Israel ikichukuwa hatua kufunga Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi hadi Jumatatu jioni kutokana na hofu ya kushambuliwa wakati wa tamasha la Purim la Kiyahudi linalokuja.

Awali jeshi la Israel limetangaza kumaliza operesheni yake ya siku tano ya kujipenyeza kwenye mji wa Ukingo wa Magharibi wa Nablus.