JERUSALEM: Kazi za ukarabati zaendelea karibu na Msikiti wa Al-Aqsa | Habari za Ulimwengu | DW | 11.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Kazi za ukarabati zaendelea karibu na Msikiti wa Al-Aqsa

Licha ya upinzani mkali,Israel imeendelea na kazi za ukarabati kwenye eneo la Msikiti wa Al-Aqsa. Wajenzi,chini ya ulinzi wa polisi wapato 2,000 walirejea kuendelea na kazi za ukarabati kwenye daraja linalotumiwa na watu wanaokwenda kwa miguu.Polisi wamesema,ili kuzuia mapambano mapya, Wapalestina chini ya umri wa miaka 45 hawaruhusiwi kwenda eneo hilo.Tangu siku kadhaa, Wapalestina wanaandamana wakisema kuwa kazi za ukarabati huenda zikahatarisha msingi wa Msikiti wa Al-Aqsa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com