1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel yavunjwa moyo na orodha ya wafungwa

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAq

Mawaziri wa Israel wameeleza kuvunjwa moyo kwao kuhusu orodha ya wafungwa wa kipalestina ambao chama cha Hamas kinata waachiliwe huru kabla mwanajeshi wa Israel anayezuiliwa na wanamgambo wa kipalestina huko Ukanda wa Gaza. Gilad Shalit, kuachiliwa.

Duru za kisiasa nchini Israel zimeieleza orodha hiyo ya wafungwa kuwa tatizo kubwa ambalo Israel haiwezi kulikubali ikisema wanamgambo wengi wamemwaga damu wa Waisraeli.

Waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert alifanya mazungumzo ya kwanza na maofisa wake wa usalama pamoja na waziri wa ulinzi Amir Peretz, kuhusu orodha hiyo ya wafungwa.

Israel imesema itaendelea kuwasiliana na Misri kuhusu swala hilo.

Ghazi Hamad, mpambe wa waziri mkuu wa serikali ya mamlaka ya Palestina, Ismail Haniyeh, amesema ikiwa Israel haitabadili msimao wake kuhusu kuwaachilia wafungwa, itabeba dhamana kwa kushindwa kufikia makubaliano.