1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Halutz amekubali dhamana ya matokeo ya vita vya Lebanon

17 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCa6

Mkuu wa majeshi ya Israel amejiuzulu,huku uchunguzi ukiendelea kufanywa kuhusu hatua za kijeshi zilizochukuliwa wakati wa vita vya Lebanon vya mwaka 2006.Dan Halutz,amekosolewa vikali kuhusu vile alivyoongoza vita hivyo dhidi ya Hezbollah nchini Lebanon.Vita hivyo vilianza baada ya Hezbollah kuwateka nyara wanajeshi 2 wa Kiisraeli katika shambulio la mpakani mnamo mwezi wa Julai mwaka jana.Operesheni ya kijeshi ya Israel,ilishindwa kufanikiwa katika malengo yake makuu mawili:yaani kuwashinda Hezbollah na kuwarejesha nyumbani wanajeshi waliotekwa nyara. Kwa mujibu wa Redio ya Jeshi la Israel,Halutz katika barua yake ya kujiuzulu amesema kuwa anachukua dhamana ya matokeo ya vita hivyo.Mapema mwezi huu Halutz alisisitiza kuwa hatongátuka madarakani.