1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Abbas na Rice wanataka amani ya kudumu

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnw

Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas na waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice wametoa mwito wa kuwa na makubaliano ya kuweka chini silaha katika Ukingo wa Magharibi uliokaliwa,sawa na yale makubaliano ya hivi karibuni kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.Siku ya Jumapili wanamgambo wa Kipalestina walikubali kusitisha mashambulio yao ya roketi dhidi ya Israel na badala yake Israel kuondosha vikosi vyake kutoka Gaza.Waziri Rice yupo Mashariki ya Kati kwa azma ya kutafuta makubaliano ya amani ya kudumu.Marekani inataka kumuimarisha rais Abbas alie na siasa za wastani na anaejikuta katika kinyanganyiro cha madaraka na chama cha Hamas kinachoongoza serikali ya Wapalestina tangu mwezi wa Machi,baada ya chama hicho kushinda uchaguzi mkuu.Rice,sasa anakutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert mjini Jerusalem.