1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JEM watishia kuwahujumu wanajeshi wa china huko Darfour

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSxM

Khartoum:

Kundi kubwa la waasi wa Darfour limetishia kuwashambulia wanajeshi wa kulinda amani wa kutoka China waliowasili jana katika eneo hilo la magharibi ya Sudan.“Msimamo wetu ni bayana,wachina hawaji kwasababu ya kuleta amani,lazma waondoke haraka“amesema hayo Abdel Aziz el Nur Asher, kamanda wa kundi la „Haki na Usawa-JEM, aliyetishia „watawaangalia wanajeshi wa China kua ni sehemu ya vikosi vya serikali ya Sudan .Kundi la mwanzo la wanajeshji 135 toka jumla ya wanajeshi 315 wa China wamewasili Darfour jana katika juhudi za kuandaa kutumwa kikosi cha kulinda amani kitakachowajumuisha wanajeshi wa Umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika-UNAMID.JEM wanaituhumu China kuitetea serikali ya Sudan katika Umoja wa mataifa.Abdelaziz el Nur Asher,ambae ni mmojawapo wa ndugu wa mkuu wa JEM KHALIL Ibrahim amesema wanajadiliana na makundi mengine ya waasi ili wawe na msimammo kama huo dhidi ya China.Kikosi cha UNAMID kinachotarajiwa kua na wanajeshi 26 elfu kinatazamiwa kuanza shughuli zakei mapema mwakani,lengo likiwa kumaliza vita vya miaka mitano vya wenyewe kwa wenyewe .