Je, United watawapa Liverpool taji la Ligi? | Michezo | DW | 22.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Je, United watawapa Liverpool taji la Ligi?

Manchester United watakuwa wanaingia katika mechi ya Ligi Kuu ya England Jumatano wakiwa wanachechemea baada ya kutandikwa mabao 4-0 na Everton uwanjani Goodison Park.

Kocha wa United Ole Gunnar Solksjaer ameghadhabishwa na kipigo hicho na kusema kuwa atakifanyia mabadiliko kikosi chake katika dirisha la uhamisho la msimu wa majira ya joto.

"Lazima tuombe msamaha kwa mashabiki wetu kwasababu leo walitushabikia kwa dhati. matokeo hayakuwa mazuri na tunajua tumewavunja moyo mashabiki wetu, ni vigumu kuelezea kwasababu matokeo ni mabaya sana," alisema Solksjaer. "Tunastahili kusalia kitu kimoja kama timu na hatuezi kukibadilisha kikosi chote kwa wakati mmoja, ni jambo linalofanyika kwa hatua. Nimesema kila mara kwamba nitafanikiwa hapa na kuna wachezaji katika kikosi cha sasa ambao hawatokuwa sehemu ya kikosi hicho kitakachopata ufanisi," aliongeza kocha huyo.

Hapo Jumapili Arsenal walishindiliwa mabao matatu kwa mawili na Crystal Palace uwanjani kwao Emirates huku Liverpool wakipata ushindi wa mbili bila walipokuwa ugenini kucheza na Cardif City.