1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUfaransa

Je, Ufaransa itaweza kutetea taji lake?

4 Desemba 2022

Jitihada za Ufaransa za kuhifadhi Kombe la Dunia zinaendelea watakapokutana na Poland huku England ikitafuta taji la kwanza kubwa katika kipindi cha miaka 56 itakabiliana na mabingwa wa Afrika Senegal.

https://p.dw.com/p/4KRlL
Fußball-WM Katar 2022 | Frankreich v Australien | Kylian Mbappe
Picha: Anne-Christine Poujoulat/AFP/Getty Images

Timu ya Ufaransa ya Didier Deschamps inalenga kuwa timu ya kwanza kushinda kombe la dunia mfululizo tangu Brazil mwaka 1958 na 1962 baada ya kushinda Kundi D nchini Qatar.

soma Ubora soka la Ujerumani wafika ukingoni?

Wakiongozwa na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe, Ufaransa imepewa nafasi kubwa ya kusonga mbele na dhidi ya Poland katika mechi itakayochezwa katika Uwanja wa Al Thumama mjini Doha.

Lakini mechi za Kombe la Dunia mwaka zimeonyesha matokeo tofauti na kuwashangaza wengi kama vile kubanduliwa kwa Ujerumani na Ubelgiji katika hatua ya makundi. Kumzuia mshambuliaji wa Barcelona Robert Lewandowski ndio ufunguo wa matumaini ya Ufaransa ya kuepuka mfadhaiko.

soma Kombe la Dunia 2022: Senegal imekuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuvuka ngazi ya makundi

Lewandoski ambaye ni mfungaji bora wa timu ya taifa ya Poland atakuwa na matumaini ya kuongeza idadi katika Kombe la Dunia dhidi ya mlinda mlango wa Ufaransa Hugo Lloris, ambaye anakaribia kufikisha mechi yake ya 142 ya kimataifa sawa na Lilian Thuram kama mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi za Les Bleus'.

Lewandowski anajukumu kubwa

Fußball Nationalspieler | Robert Lewandowski  Polen
Picha: Darren Staples/CSM/Zuma/picture alliance

Nahodha wa Ufaransa Lloris aliwasifu Lewandowski na mwenzake wa Poland Wojciech Szczesny, ambaye amefanya vyema kwa kuokoa mikwaju miwili ya penalti ambayo ilikuwa muhimu kwa timu yake kumaliza nafasi ya pili katika Kundi C.

"Lewandowski amekuwa mmoja wa nambari tisa bora duniani kwa miaka sasa, ni timu nzuri kwa ujumla,"  "Szczesny ana mchuano mzuri, Poland walifuzu kutinga hatua ya 16 bora kutokana na weledi wa kipa wao." alisema Lloris.

Ikiwa Ufaransa itaitoa Poland, njia yao ya kuelekea fainali ya Kombe la Dunia mnamo Desemba 18 inaweza kujumuisha pambano la robo fainali dhidi ya England.

Kikosi cha Gareth Southgate kinatazamiwa kukutana na Ufaransa katika hatua ya nane bora ikiwa wataifunga Senegal kwenye Uwanja wa Al Bayt.

England ilifika nusu fainali miaka minne iliyopita na kumaliza washindi wa pili kwenye Euro 2020, na walianza vyema Qatar kwa kushinda mechi zao kwenye Kundi B. Na wanaamini kuwa wanaweza kushinda mashindano hayo huko Qatar na hatimaye kufikia ukomo kusubiri kwao kwa uchungu kwa taji la kwanza kuu tangu Kombe la Dunia la 1966.

"Hiyo sio kujiamini kupita kiasi, huo ni unyenyekevu wa kutosha kuona kinachoendelea katika mazoezi yetu na jinsi wafanyikazi wanavyojiandaa, na kujiamini pia," beki wa Uingereza John Stones alisema.

Wakiwa wametikiswa na jeraha la mchezaji Sadio Mane kabla ya mchuano wao, Senegal ilifuzu kwa hatua ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa mara ya pili baada ya ushindi wa Jumanne wa 2-1 dhidi ya Ecuador na kujihakikishia nafasi ya pili katika Kundi A.

Messi afunga bao lake la 789

FIFA WM 2022 Katar | Achtelfinale | Argentinien vs Australien
Picha: Nigel Keene/firo Sportphoto/picture alliance

Siku ya Jumamosi Lionel Messi alisaidia kupanga pambano la robo fainali na Uholanzi, washinda wa 3-1 dhidi ya Marekani. Messi aliifanya Argentina kuibuka na hisia nyingi mbele ya halaiki ya mashabiki kwa kupachika bao lake la 789 katika mechi yake ya 1,000 katika maisha yake ya soka, ikiwa ni mara yake ya kwanza katika mechi ya mtoano ya Kombe la Dunia.

"Ninajua juhudi wanazofanya ili kuwa hapa pamoja nasi na najua jinsi walivyofurahia, Kuna uhusiano tulionao-- ni kitu kizuri, ndivyo timu ya taifa inavyopaswa kuwa." alisema Messi kuhusu wafuasi wa timu yake.

Messi alianza kufunga dakika ya 35 ya mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Ahmad bin Ali. Bao lake lilionekana kuwaweka Argentina kwenye njia ya kupata ushindi mnono, hasa baada ya Julian Alvarez kugongesha makosa ya mlinda mlango wa Australia Mathew Ryan na kuongeza bao la pili la timu yake.