Je rais Bush atakubali kusaini mpango wa kupunguza Carbon? | Habari za Ulimwengu | DW | 08.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Je rais Bush atakubali kusaini mpango wa kupunguza Carbon?

-

TOYAKO

Wajumbe wa kundi la nchi za G8 wamefikia makubaliano juu ya mapendekezo ya majaribio kuhusu njia za kukabiliaana na ongezeko la ujoto duniani ambayo yatawasilishwa hii leo mbele ya viongozi wakuu wa nchi hizo.Maafisa wakuu wa nchi hizo waliokutana katika kikao maalum jana usiku walijadiliana kuhusu mapendekezo ambayo yataifanya Marekani kulazimika kutia saini makubaliano ya kupunguza utoaji wa gesi chafu kufikia katikakati ya karne hii.Rais Bush anakabiliwa na shinikizo kutoka Japan na Umoja wa Ulaya kuhusiana na mpango huo lakini amesisiza kwamba hawezi kukubaliana nao hadi pale mataifa ya China na India ambayo yanatoa gesi chafu kwa wingi yatakapokubali kupunguza utoaji wa gesi chafu ya Carbon.Aidha hapo jana rais wa benki ya dunia Robert Zoellick akizungumza kandoni mwa mkutano wa G8 alitaka pafanyike mageuzi katika sera za nishati mbadala katika nchi tajiri na kuzitolea mwito kukuza zaidi mazao ya chakula kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa chakula duniani.Na kwa upande mwingine katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon alizitolea mwito nchi hizo tajiri kuzitatua changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na bei za vyakula pamoja na suala la maendeleo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com