1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, hatua ya kuungana Ujerumani ilichukuliwa mapema?

Saumu Mwasimba
31 Oktoba 2019

Baada ya kuporomoshwa kwa ukuta wa Berlin Wajerumani milioni 17 wa Ujerumani Mashariki na milioni 64 kutoka Ujerumani Magharibi hatimae waliweza tena kupeana mikono.

https://p.dw.com/p/3SDP7
Berlin | East Side Gallery
Picha: picture-alliance/imageBROKER/J. Woodhouse

Baada ya kuporomoshwa kwa ukuta wa Berlin Wajerumani milioni 17 wa Ujerumani Mashariki na milioni 64 kutoka Ujerumani Magharibi hatimae waliweza tena kupeana mikono.

Lakini kwa wengi kuungana huku kwa Ujerumani mbili kumefanyika mapema mno na kinachowafanya wengi kuhisi hivyo ni kwa sababu kwanza Ujerumani Magharibi ndiyo inayotawala na sheria zake ndizo zilizohamishiwa mpaka upande wa Mashariki. Kwa wakaazi wengi wa Mashariki mabadiliko hayo ni ya ghafla mno waliyokumbana nayo. Walijikuta kwenye shinikizo kubwa la kutakiwa kubadilisha mifumo yote na hata   nyaraka za wasifu za baadhi ya watu zilionekana kupoteza hata maana.

10482 Die Mauer, unsere Familie und wir 2
Picha: DW

Na hata wakati huu sio siri kwamba watu wa Ujerumani Magharibi hawana muda wa kuangalia wasifu wa watu kutoka upande wa pili yaani Mashariki. Juu ya hilo wako wajerumani ambao hawajawahi hata siku moja kukanyaga ardhi ya upande wa pili wa nchi hii.

Majina ya kebehi kama Ossi,ikimaanisha watu kutoka Mashariki na Wessi, watu kutoka Magharibi ni sehemu ya maneno ambayo bado yanatumiwa na kusikika kwenye vinywa vya watu ambao fikra zao bado zimetawaliwa na kumbukumbu za sura ya ukuta wa Berlin. Hali hii inahusiana pia na tafauti ya maisha yaliyokuwepo wakati huo na hivi sasa.

Inafahamika kwamba upande wa Mashariki hali ilikuwa ni ya umasikini na hata wakati huo bado umasikini huo upo wakati upande wa Magharibi kiwango cha mishahara kiko juu. Ili kuiondowa tafauti hiyo walipa kodi wanalipa kile kinachoitwa kodi ya mshikamano ambayo tayari inagharimu mamia ya mabilioni ya Yuro.

Deutschland | Berlin | Gedenkstätte Bernauer Straße
Picha: DW/L. Jordan

Suala hili baadhi ya wakati linasababisha wivu upande wa Magharibi na hasa pale inapotokea kuna miundo mbinu mbovu katika maeneo kadhaa inaibuka mijadala ya kujadili miradi ya ujenzi inayofanyika Mashariki. Dhima kubwa inayoleta utata katika suala la Ujerumani kuungana tena imeletwa na kile kinachofahamika kama ,''Treuhand'' ambapo makampuni 8000 Kutoka Mashariki yalikuja pamoja na kuondoka na wafanyakazi wake milioni nne.

Hili ni suala ambalo limesababisha hali ya kiuchumi ya Mashariki kuporomoka na idadi kubwa ya makampuni kulazimika kufunga milango yao. Na sababu kubwa ni kwamba mengi yalishindwa kuingia kwenye ushindani na upande wa Magharibi na watu wengi walipoteza ajira. Hali hiyo imeshuhudiwa mpaka mwaka 2005 alipoingia madarakani Kansela Angela Merkel ambaye binafsi ametokea Mashariki. Katika kipindi hicho yalianza kuonekana maendeleo ya kiuchumi katika kipindi cha muongo mmoja ikiwemo eneo hilo la Mashariki.

Mwandishi: Saumu Mwasimba/Scholz-Key Alexander

Mhariri: Grace Patricia Kabogo