JAPAN:Soko la hisa ulimwenguni laendelea kuporomoka
16 Agosti 2007Matangazo
Soko la hisa ulimwenguni linaendelea kuporomoka kutokana na mgogoro wa mikopo nchini Marekani.
Thamani ya hisa katika masoko ya ulaya imeshuka kwa miezi mitano mfululizo.
Masoko ya hisa ya Frankfurt, London na Paris yameripoti biashara duni na kushuka thamani kwa kiwango cha asilimia mbili au zaidi.
Masoko ya hisa ya bara Asia pia yameripoti hasara.
Hali hiyo imesababisha wawekezaji vitega uchumi wakimbilie katika sekta tulivu kama kuwekeza kwenye hisa za seirkali.