Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kusaidiwa kupambana na waasi | Habari za Ulimwengu | DW | 05.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kusaidiwa kupambana na waasi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Condoleezza Rice ameahidi kuimarisha vikosi vya usalama vya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo vinavyopigana dhidi ya waasi na majeshi ya kigeni.Waziri Rice yupo Addis Ababa nchini Ethiopia kwa majadiliano pamoja na wajumbe wa Umoja wa Afrika na marais wa eneo la Maziwa Makuu.

Kiini cha majadiliano hayo ni mapigano nchini Somalia,Sudan na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Sudan imelaumiwa na Umoja wa Matifa kwa kutowalinda wakaazi wa jimbo la Darfur dhidi ya mashambulizi ya waasi,vikosi vya serikali na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali.Tangu mwaka 2003,zaidi ya watu 200,000 wameuawa katika jimbo la Darfur.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com