Jamaa wa waandishi wanaozuiliwa hawataonana Iran | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 27.12.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Jamaa wa waandishi wanaozuiliwa hawataonana Iran

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imeeleza kuwa hakuna uwezekano wowote wa waandishi wa habari wanaozuiliwa Iran kukutana na jamaa zao waliokwenda kuwatembelea.

default

Sakineh Mohammadi Ashtiani aliyehukumiwa kifo kwa kupigwa mawe.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani,jamaa hao hawataweza kukutana katika kipindi hiki cha Krismasi kama walivyoahidiwa na serikali ya Iran.

Mostafaie auf der Pressekonferenz

Wakili wa Sakineh Mohammadi akifanya mkutano na waandishi wa habari mwezi wa Agosti.

Awali,akihojiwa na Gazeti la Bild Am Sonntag,Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Guido Westerwelle,alisema kuwa huenda wakakutana wakati huu.Waandishi hao wawili wa habari wa gazeti la Bild Am Sonntag walikamatwa mwezi wa Oktoba walipouwa wakiwahoji mtotto wa kiume na wakili wa Sakineh Mohammadi Ashtiani aliyehukumiwa kifo kwa kupigwa mawe.Mwanamke huyo aliye na umri wa miaka 43 alikatiwa hukumu hiyo kwasababu ya mashtaka ya zinaa.Waandishi hao wa habari waliingia Iran kw akutumia vibali vya watalii.

 • Tarehe 27.12.2010
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/zq4E
 • Tarehe 27.12.2010
 • Mwandishi Thelma Mwadzaya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/zq4E
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com