JAKARTA.Ziara ya Bush yakumbwa na maandamano makubwa | Habari za Ulimwengu | DW | 20.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JAKARTA.Ziara ya Bush yakumbwa na maandamano makubwa

Rais George W Bush wa Marekani yuko nchini Indonesia kwa ziara fupi nchini humo lakini inayokabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi.

Kabla ya kuwasili kiongozi huyo watu kadhaa walimiminika katika mabarabara ya mji mkuu wa Jakarta kupinga sera za mambo ya nje za Marekani, hususan kuhusu vita vya Irak na Afghanistan na mzozo wa mashariki ya kati.

Rais Bush katika ziara yake ya masaa sita atakutana na rais Susilo Bambang Yudhoyono na maafisa wa vyeo vya juu wa Indonesia.

Hali ya usalama imeimarishwa zaidi katika nchi mashuhuri ya kiisalmu ya Indonesia wakati huu wa ziara ya rais Bush.

Kabla ya ziara yake ya nchini Indonesia rais Bush alihudhuria mkutano wa viongozi wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia na Pacific APEC uliofanyika mjini Hanoi nchini Vietnam.

Mkutano wa Hanoi umesisitiza azma ya kuyafufua mazungumzo ya duru ya Doha juu ya biashara duniani yaliyoviunjika mwezi julai.

Katika mkutano huo wa siku mbili Urusi na Marekani zilitia saini mkataba wa maelewano ambao sasa umeifungulia njia Urusi kujiunga na shirika la biashara duniani WTO.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com