JAKARTA.Watu wawili zaidi wafa kwa ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege | Habari za Ulimwengu | DW | 16.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JAKARTA.Watu wawili zaidi wafa kwa ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege

Watalaamu wa Afya nchini Indonesia wamesema watu wawili zaidi wamekufa na ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege.

Hadi sasa watu 54 wameshakufa baada ya kuambukizwa virusi vya N5N1 vinavyo sababisha homa ya mafua ya ndege nchini Indonesia.

Mwanamke wenye umri wa miaka 67 kutoka eneo la Bandung katika kisiwa cha Java amekufa baada mtoto wa miaka kumi na moja kufa siku mbili zilizopita katika mji wa Jakarta.

Madaktari wamethibitisha kuwa mtoto huyo alikuwa karibu na mifugo ya ndege.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com