1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Tetemeko la ardhi nchini Indonesia

16 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrL

Tetemeko kubwa la ardhi lenye nguvu ya 6.1 kwenye Kipimo cha Richter limetokea kwenye Visiwa vya Maluku vya Indonesia,kaskazini-mashariki ya nchi.Msemaji wa Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa,akizungumza mji mkuu wa Indonesia,Jakarta amesema,kiini cha tetemeko hilo kilikuwa kama kilomita 39 chini ya uvungu wa bahari.Akaongezea kuwa hakuna ripoti juu ya hasara iliyosababishwa na tetemeko hilo la ardhi.