JAKARTA: Kiongozi wa wanamgambo wa Kiislamu akamatwa Indonesia. | Habari za Ulimwengu | DW | 16.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JAKARTA: Kiongozi wa wanamgambo wa Kiislamu akamatwa Indonesia.

Maafisa wa usalama nchini Indonesia wamesema wamemtia nguvuni Zarkasih anayesemekana kuwa kiongozi wa kundi la Jemaah Islamiya.

Mkuu wa kitengo cha kukabiliana na ugaidi nchini humo amesema Zarkasih alikamatwa mwishoni mwa juma lililopita.

Maafisa hao wa usalama wametoa tangazo hilo siku moja baada ya kutangaza wamemkata Abu Dujana ambaye pia ni kiongozi mkuu wa kundi hilo la Jemaah Islamiya.

Duru za kiusalama zinasema kundi hilo la wanamgambo wa kiislamu limepata pigo kubwa kutokana na kukamatwa kwa viongozi hao.

Kundi la Jemaah Islamiya linasemekana ndilo lililotega mabomu mjini Bali mwaka 2002, mabomu yaliyosababisha vifo vya watu mia mbili na wawili wakiwemo raia themanini na wanane wa Australia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com