1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Istanbul. PKK wauwa wanajeshi 13 wa Uturuki.

8 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ha

Wapiganaji wa Kikurdi kutoka katika kundi linalotaka kujitenga la PKK, wamewauwa wanajeshi 13 wa Uturuki katika shambulio lililofanyika karibu na mpaka wa nchi hiyo na Iraq.

Ni moja kati ya hasara kubwa iliyopata jeshi la Uturuki katika mapigano na kundi hilo. Ripoti zinasema kuwa ni mpiganaji mmoja tu wa kundi la PKK aliyeuwawa. Jeshi la Uturuki lilishambulia kwa makombora eneo la mpaka katika juhudi za kuwazuwia wapiganaji kukimbilia eneo la kaskazini mwa Iraq. Akizungumzia tukio hilo jenerali wa zamani wa jeshi la Uturuki Haldun Solmaztürk amesema nchi hiyo inapaswa kuchukulia kwa tahadhari tukio hilo.

Serikali ya Uturuki inasema kuwa kiasi cha wapiganaji 3,000 wa PKK wanamakao yao katika eneo linalodhibitiwa na Wakurd kaskazini mwa Iraq.