1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maadhimisho ya Israel

Mtullya, Abdu Said8 Mei 2008

Maadhimisho ya miaka 60 tokea kuundwa nchi ya kiyahudi-Israel yanaendelea .

https://p.dw.com/p/Dwau
Aliekuwa kansela wa Ujerumani Konrad Adenauer na waziri mkuu wa kwanza wa Israel Ben-GurionPicha: dpa


Isreal  inaadhimisha  mwaka wa 60 tokea kuundwa  baada ya kupitia mitihani mizito  katika historia yake.

Lakini imeweza  kuhimili mitihani hiyo.


Waisraeli  wanaadhimisha mwaka  wa 60 wa nchi yao kwa sherehe mbalimbali ikiwa pamoja  na  hotuba  za  viongozi kuwapongeza  na kuwakumbuka waasisi wa wa nchi hiyo.Sherehe zilianza  kwa  kupandisha  bendera kwenye mlima  wa Herzl  uliopo Jerusalem.Majeshi ya usalama  yalikuwa katika  hali ya tahadhari kutokana na wasiwasi  mashambulio ya wapiganaji wa kipalestina.

Wakati Israel  inaadhimisha miaka 60 tokea  kuundwa, wapalestina wanajitayarisha  kuadhimisha miaka 60 ya wanachoita "Nakba" maafa.

Israel  imejengwa na watu  wa  taifa jipya na la zamani baada ya kukumbwa na maafa makubwa barani Ulaya.

Utawala  wa  mafashisti nchini Ujerumani ulianzisha kampeni ya kuwaangamiza wayahudi milioni sita barani Ulaya.

Na hata  baada  ya Israel kuundwa nchi hiyo imepitia mitihani mizito kutokana na uhasama na jirani zake- nchi za kiarabu.

Lakini nchi hiyo imeweza kuhimili mitihani hiyo mizito. Kwani tokea kuundwa kwake miaka  60 iliyopita waisraeli wameshapigana vita mara kadhaa na jirani zao.

Maalfu  ya waisrael mjini Jerusalem wanashiriki katika  maadhimisho ya nchi yao wakati  ambapo mustakabal wa kisiasa  wa  waziri mkuu wa nchi hiyo bwana Ehud  Olmert umo  mashakani kutokana na kukabiliwa na tuhuma za ufisadi.

Akiwapongeza waisraeli katika madhimisho ya taifa lao rais  wa Ujerumani  Horst Köhler amesisitiza kuwa kuendelea  kuwapo  kwa taifa la Israel  ni nyanja  ya msingi katika sera ya nje ya Ujerumani. Rais Köhler amesema Ujerumani wakati wote itasimama kutetea  haki ya waisraeli ya kuishi maisha ya amani. Lakini pia ameeleza kuwa msingi wa amani ya kudumu katika  mashariki ya kati ni kukomeshwa umwagikaji damu.