1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia vituo katika Ukanda wa Gaza

5 Septemba 2010

Mashambulio matatu ya jeshi la anga la Israel yamelenga vituo vya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/P4ii
A Palestinian man inspects the damage following Israeli air strikes on a smuggling tunnel at the border with Egypt in Rafah refugee camp, southern Gaza Strip, Sunday, Sept. 5, 2010. One Palestinian was killed, a second was wounded and three more were missing, Hamas security officials said Sunday, as Israeli aircraft bombed a Gaza smuggling tunnel in retaliation for Hamas shooting attacks. (AP Photo/Eyad Baba)
Uharibifu uliosababishwa na shambulio la Israel dhidi ya njia ya chini kwa chini kwenye mpaka wa Misri na Ukanda wa Gaza.Picha: AP

Mtu mmoja aliuawa na wengine watatu walijeruhiwa katika mashambulio mawili dhidi ya njia inayopitia chini kwa chini kuelekea Misri ambayo hutumiwa kwa biashara haramu.

Shambulio la tatu lililenga ngome ya zamani ya kundi la Hamas katika mji wa Khan Yunis ulio kusini mwa Ukanda wa Gaza. Jeshi la Israel limethibitisha kufanya mashambulio hayo.Imechukua hatua hiyo kujibu mashambulio mapya ya makombora yaliyolenga makaazi ya Wayahudi hivi karibuni kutoka kusini mwa Ukanda wa Gaza.

After speaking to the media on the progress of Middle East peace talks in the East Room of the White House, Palestinian Authority President Mahmoud Abbas (L) chats with Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu (R) in Washington, DC, USA, on 01 September 2010. On 02 September, the Middle East leaders will meet again, this time at the State Department with Secretary Hillary Clinton. EPA/MOSHE MILNER GOVERNMENT PRESS OFFICE HANDOUT ISRAELI MEDIA MUST CREDIT GPO, EDITORIAL USE ONLY / NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu (kulia), baada ya mkutano wao na waandishi wa habari mjini Washington,01 Septemba, 2010.Picha: picture-alliance/dpa

Siku ya Alkhamisi Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas, walikutana ana kwa ana kwa mazungumzo ya amani mjini Washington. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa viongozi hao kukutana ana kwa ana baada ya majadiliano ya amani kuvunjika takriban miaka miwili iliyopita.