1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yapania kujenga makazi mapya ya walowezi wa kiyahudi

12 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D6ZI
Serikali ya Israel inapanga kujenga makaazi mapya takriban 1,100 ya walowezi wa kiyahudi mashariki mwa mji wa Jerusalem. Waziri wa ujenzi wa Israel, Seev Boim, amesema kandarasi za ujenzi wa makaazi hayo zitatangazwa hivi karibuni. Katika mpango huo makaazi 370 yatajengwa katika kitongoji cha Har Homa na mengine 750 katika kitongoji cha Pisgat Seev mashariki mwa Jerusalem. Miezi miwili iliyopita Israel ilitangaza ujenzi wa makazi 350 katika kitongoji cha Har Homa na kusababisha ukosoaji mkubwa miongoni mwa wapalestina na jumuiya ya kimataifa. Wapalestina wanaamini Jerusalem Mashriki itakuwa mji mkuu wa taifa huru la Palestina litakaloundwa katika siku za usoni.