1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yapanga kujenga makaazi mapya Jerusalem

Abdu Said Mtullya30 Mei 2013

Mjumbe wa kimataifa wa Wapalestina Saeb Erakat amesema mpango wa Israel wa kujenga makaazi mengine 1000 mashariki mwa Jerusalem utazikwamisha juhudi za kuyafufua mazungumzo ya kuutatua mgogoro wa Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/18hJ4
Wapalestina wapinga kutekwa kwa maeneo yao
Wapalestina wapinga kutekwa kwa maeneo yaoPicha: Reuters

Erakat aliitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya asasi moja kuarifu kwamba Israel inapanga kujenga makaazi zaidi ya walowezi.

Erakat amesema mpango wa Israel wa kujenga makaazi zaidi katika Jerusalem ya Mashariki utazivuruga kabisa juhudi zinazofanywa na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry za kuufufua mchakato wa kuleta amani katika Mashariki ya Kati.

Erakat ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Israel ina mpango wa makusudi wa kuzivuruga juhudi za Waziri Kerry. Amesema inapohusu kuchagua biana ya makaazi mapya na amani, Israel wakati wote imechagua kuendelea na ujenzi wa makaazi mapya katika maeneo ya Wapalestina.

Kandarasi za ujenzi zatiwa saini:

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali nchini Israel bwana Danny Seidemann aliliambia shirika la habari la AFP kwamba kandarasi kwa ajili ya nyumba 300 katika kitongoji cha Ramot kaskazini mashariki mwa Jerusalem tayari zimeshatiwa saini na viwanja 797 vitauzwa kusini mwa Jerusalem katika kitongojo cha Golo kilichopo karibu na Ukingo wa Magharibi.

U.S. Secretary of State John Kerry (L) meets with Israeli Prime Minster Benjamin Netanyahu in Jerusalem May 23, 2013. REUTERS/Jim Young (ISRAEL - Tags: POLITICS)
Jonh Kerry und Benjamin Netanjahu wakiwa JerusalemPicha: Reuters

Vitongoji hivyo viwili vipo katika maeneo ambayo hasa ni ya Waarabu katika mji huo wa Jerusalem. Vitongoji hivyo vilitekwa na Israel katika vita vya siku sita vyamwaka wa 1967 na baadae kuwekwa chini ya himaya ya Israel, hatua ambayo mpaka leo haijatambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

Mkurugenzi wa asasi iliyotoa taarifa juu ya ujenzi wa makaazi mapya bwana Seidemann amesema mipango ya ujenzi ilishapitishwa mwaka uliopita kabla ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuagiza kimya kimya kusimamisha kwa muda ujenzi wa makaazi. Lakini habari juu ya mipango ya ujenzi wa makaazi hayo 1000 zimepenya kwa vyombo vya habari.

Netanyahu ajaribu kuepuka lawama:

Ingawa hatua ya kusimamisha ujenzi kwa muda ,haikuthibitishwa rasmi, mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Israel yamesema, Netanyahu hakutaka kuonekana kuwa ni pingamizi la juhudi za Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry za kuyafufua mazungumzo baina ya Israel na Wapalestina

Wapalestina wanaitaka Israel iache kabisa shughuli za ujenzi wa maakazi mapya katika maeneo yao ili mazungumzo yaweze kuanza tena.

Mwandishi:Mtullya Abdu.Aptn,afp,

Mhariri:Mohammed Abdul-rahman