Israel yaendelea kuihujumu Gaza | Matukio ya Kisiasa | DW | 11.07.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Israel yaendelea kuihujumu Gaza

Madege ya kivita ya Israel yanaendelea kuuhujumu Ukanda wa Gaza kwa siku ya nne mfululizo bila ya kufanikiwa kuzuwia makombora yanayfyetuliwa na makundi ya wanamgambo wa kipalastina..

Mabomu ya Israel yapiga Rafah

Mabomu ya Israel yapiga Rafah

Zaidi ya wapalastina 80 wameuuliwa tangu jumanne iliyopita katika eneo hilo linalozingirwa,wengi wao ni raia.Madege ya Israel yameushambulia alfajiri ya leo mji wa Gaza na ule wa Rafah na kuangamiza maisha ya watu wasiopungua wanne.

Kombora la wanamgambo wa kipalastina limepiga katika kituo cha kuuza mafuta katika mji wa Israel wa Ashdod na kusababisha mripuko mkubwa na kuwajeruhi watu wasiopungua watatu.

Jeshi la Israel limesema wanaanga na wanamaji wamehujumu vituo kadhaa bila ya kutoa maelezo zaidi.Kwa jumla jeshi la Israel linasema limehujumu vituo 860 katika Ukanda wa Gaza.

Akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni jana usiku waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema:" Tumewapiga Hamas na magaidi na kwa wakati wote ambao kampeni hii inaendelea tutaendelea kuwahujumu."

Ameshadidia waziri mkuu wa Israel aliyepuuza pendekezo la rais Barack Obama la kutaka kupatanisha.

Katika mazungumzo ya simu kati ya rais Barack Obama na waziri mkuu wa Israekl Benjamin Netanyahu,rais Obama alisema Marekani iko tayari kurahisisha kuondowa uhasama ikiwa ni pamoja na kurejeshwa makubaliano ya kuwekwa chini silaha yaliyofikiwa Novemba mwaka 2012.

Wapalastina wanaasema hawatoondoka

Palästinenser versuchen von Gaza nach Ägypten zu kommen 10.7.2014

Wapalastina wanajaribu kukimbilia Misri

Katika wakati ambapo Israel inatishia kutuma vikosi vya nchi kavu waziri wa ulinzi Moshe Yaalon anasema wanajiandaa kwa mapambano ya muda mrefu kutokana na kuzidi kufyetuliwa makombora na Hamas.

Makombora matatu yaliyofyetuliwa kutoka Gaza yameteketezwa na mtambo wa kukinga hujuma za makombora Iron Dome,huko Tel Aviv. Na kombora lililofyetuliwa toka kusini mwa Libnan limepiga kaskazini ya Israel lakini bila ya kusababisha hasara yoyote.

Hujuma za mabomu ya Israel hazijafanikiwa hadi sasa kukomesha makombora ya Hamas.

Msemaji wa Hamas huko Gaza,Sami Abou Zouhri anasema tunanukuu:" tumebanwa,hatuna cha kupoteza.

Kwa upande wake kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina mahmoud Abbas anasema:"Wanataka tuihame nchi yetu,lakini hatutoondoka.hatuna silaha,lakini tutapigana kwa kutumia macho yetu,tutapigana kwa maneno".

Israel yaadhibu waaliomo na wasiokuwemo

Gaza Zerstörung Luftangriffe aus Israel 10.7.

Majumba ya wapalastina yateketezwa kwa mabomu ya Israel

Misri pia imelaani "mtindo wa Israel wa kuwaadhibu waliomo na wasiokuwemo na kuitolea wito jumuia ya kimataifa ikomeshe haraka ugonvi huu ulioangamiza maisha ya karibu watu 100 haadi sasa.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com