Israel na Palestina zaonywa kuhusu Jerusalem | NRS-Import | DW | 16.01.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

NRS-Import

Israel na Palestina zaonywa kuhusu Jerusalem

Mkutano juu ya amani Mashariki ya Katiti uliofanyika Paris Jumapili (16.01,2017)umezionya Israel na Wapalestina dhidi ya kuchukuwa hatua za upande mmoja kuhusu mji wa Jerusalem na mipaka.

Takriban nchi 70 imezitaka pande hizo mbili kuepuka hatua ambazo zitahukumu kabla matokeo ya mazungumzo juu ya masuala ya mwisho ikiwemo hadhi ya mji wa Jerusalem, mipaka, usalama na wakimbizi.

Washiriki wa mkutano huo hawatozitambua hatua hizo, wameonya katika taarifa. Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa ameuambia mkutano huo wa waandishi habari kwamba pia wamekubaliana msingi wa mazungumzo unapaswa kuwa mipaka iliokuwepo mwaka 1967 kabla ya Israel kukalia kwa mabavu Ukingo wa Magharibi na Jerusalem ya mashariki.

Israel na Palestina hawakuhudhuria mkutano huo ambao Wapalestina wanauunga mkono lakini Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameuupuzilia mbali kuwa hauna tija.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akihudhuria mkutano huo katika ziara yake ya kuaga amesema alizungumzia kuzuwiya kutotendewa haki kwa Israel.

Sulushisho la urari

Paris Nahost Konferenz (Getty Images/AFP/B. Guay)

Rais Francois Hollande wa Ufaransa akisalimiana na viongozi waliohudhuria mkutano wa Paris.

Kerry amesema wamefanya kile inachobidi ili kuwa na suluhisho lenye urari na kwamba amezungumza na Netanyahu wakati wa mkutano huo ili kumhakikishia hilo.

Kerry amesema kwamba mataifa makuu ya Kiarabu yameidhinisha mpango wa Marekani kufikia suluhisho ambao unasisitiza juu ya haja ya kuwepo kwa mataifa mawili mojawapo ni kutambuliwa kwa Israel kama taifa la Kiyahudi.

Wapalestina wameikaribisha taarifa ya kufunga mkutano huo ambapo Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Wapalestina (PLO) Saeb Erekat amesema imesisitiza haja ya kukomesha hatua ya Israel kuikalia kwa mabavu ardhi ya Wapalestina.

Hata hivyo Israel imesema mkutano huo na mengine kama hiyo inafanya iwe vigumu kupatikana kwa amani kwa kuwa inawashajiisha Wapalestina waendelee kususia mazungumzo ya moja kwa moja na Israel.

Mkutano huo unakuja wakati Rais Mteule wa Mrekani Donald Trump akiahidi katika kampeni zake kuhamishia Jerusalem ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv jambo ambalo limezusha wasi wasi mkubwa wa kupatikana kwa amani Mashariki ya Kati kwani itamaanisha kuutambuwa mji huo unaozozaniwa kuwa ni mji mkuu wa Israel.

Mwandishi : Mohamed Dahman/AFP

Mhariri: Iddi Ssessanga

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com