Israel na Hezbollah wasaini mapatano ya kubadilishana wafungwa | Habari za Ulimwengu | DW | 08.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Israel na Hezbollah wasaini mapatano ya kubadilishana wafungwa

-

JERUSALEM

Israel na kundi la Hezbollah wametia saini makubaliano juu ya kubadilishana wafungwa yaliyosimamiwa na Umoja wa mataifa mwezi uliopita.Tarehe ya kuanza zoezi hilo itatolewa wiki hii.Taarifa kutoka serikali ya Israel zimefahamisha kwamba makubaliano hayo yametiwa saini mbele ya wawakilishi wa Umoja huo wa mataifa.Kwa mujibu wa makubaliano hayo ni kwamba Israel itamkabidhi kwa Hezbollah mwanachama wake Samir Kuntar ambaye amehusika na mauaji mara mbili,pamoja na wafungwa wengine wanachama wa kundi hilo na pia miili kadhaa ya wanamgambo wa Hezbollah.Jana jeshi la Israel lilianza shughuli ya kuifukua miili ya wapiganaji 190 wa kundi hilo la Hezbollah.Kwa upande mwingine Israeli itakabidhibiwa wanajeshi wake wawili waliotekwa nyara na kundi hilo mwaka 2006.Wote wawili inaaminika waliuwawa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com