Israel kuongeza mashambulio Gaza | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 07.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Israel kuongeza mashambulio Gaza

---

GAZA

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema ataongeza mashambulio dhidi ya wanamgambo wanaorusha roketi ndani ya ardhi ya Israel.Matamshi ya Olmert yametoka siku ambayo mashambulio ya angani ya Israel yameua raia watatu wapalestina katika eneo linalodhibitiwa na Hamas, ukanda wa Gaza.

Shambulio hilo limeongeza hali ya wasiwasi kabla ya ziara ya rais George Bush wa Marekani itakayoanza jumatano.Ziara hiyo itakuwa ya kwanza kwa rais huyo wa Marekani nchini Israel na Palestina inayofanyika baada ya mkutano wa kilele wa mwezi Novemba kuhusu Mashariki ya kati ulioandaliwa mjini Annapolis Marekani ambapo waziri mkuu Olmert na rais Mahmoud Abbas wa Palestina waliahidi kujaribu kuyafikia makubaliano ya amani kufikia mwishoni mwa mwaka 2008.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com