1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kugawana ardhi na Palestina.

18 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CdJv

Jerusalem. Mtu wa karibu wa waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema leo kuwa Isreal inaendelea na ujenzi wa makaazi makubwa ya walowezi wa Kiyahudi katika eneo la ukingo wa magharibi , lakini inapendekezwa kuwapa fidia Wapalestina kwa kuwapa maeneo ya Israel chini ya makubaliano ya mwisho ya amani. Matamshi hayo yaliyotolewa na makamu wa waziri mkuu Haim Ramon ni ya mara ya kwanza kwa kiongozi wa Israel kuidhinisha wazi dhana ya kubadilishana ardhi. Rais wa palestina Mahmoud Abbas pia anaunga mkono dhana hiyo , lakini mjini Paris jana amesema ubadilishanaji wowote utahitaji Israel kutoa kiasi sawa kama inayochukua, lakini pia ameongeza kuwa ni mapema mno kuweza kujadili mpango kama huo.