Israel itajenga makaazi mapya Jerusalem ya Mashariki | Matukio ya Kisiasa | DW | 09.11.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Israel itajenga makaazi mapya Jerusalem ya Mashariki

Serikali ya Israel itaendelea kujenga makaazi mapya katika eneo la Waarabu mjini Jerusalem ya Mashariki.

A general view of the east Jerusalem neighborhood of Ramat Sholmo, Wednesday, March 10, 2010. Israel's new plan to build 1,600 homes for Jews in Palestinian-claimed east Jerusalem overshadowed Vice President Joe Biden's visit to the West Bank on Wednesday. Biden was to hold talks with Palestinian President Mahmoud Abbas and Prime Minister Salam Fayyad, in part to ease their doubts about the latest U.S. peace efforts. (AP Photo/Dan Balilty)

Makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika Jerusalem ya Mashariki.

Wizara ya mambo ya ndani imetangaza mradi wa kujenga nyumba 1.300. Tangazo hilo limetolewa wakati usio mzuri kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Hivi sasa yupo Marekani kwa majadiliano ya kutafuta njia ya kufufua majadiliano ya amani pamoja na Wapalestina yaliyokwama.

Msemaji wa serikali ya Marekani, amesema kuwa Washington imesikitishwa sana na tangazo hilo. Nae mpatanishi mkuu wa Wapalestina, Saeb Erekat amesema, mradi wa kuendelea na ujenzi wa makaazi ya Wayahudi katika ardhi ya Waarabu, unalenga kuvuruga mchakato wa amani.

Wakati huo huo,Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle ametoa mwito kwa Israel kuondosha vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Ukanda wa Gaza tangu miaka minne iliyopita. Amesema, kuwazingira kiasi ya watu milioni 1.5 ni hali isiyokubalika. Vile vile hiyo inaimarisha itikadi kali na ni kizuizi kwa majadiliano ya amani yanayotafuta ufumbuzi wa mataifa mawili.

German Foreign Minister Guido Westerwelle stands between refugees student girl in the class during his visit to Al Shatea school in the west of Gaza City on, 09 November 2010. Westerwelle is on an official visit to Israel and the Palestinian territories. EPA/MOHAMMED SABER

Waziri Westerwelle wa Ujerumani, alipotembelea shule ya wasichana katika Ukanda wa Gaza.

Wakati wa ziara yake hiyo fupi katika Ukanda wa Gaza, waziri Westerwelle alikataa kukutana na maafisa wa Hamas wanaodhibiti eneo hilo.Waziri huyo akatoa mwito kwa Wapalestina kumuachilia huru mwanajeshi wa Kiisraeli Gilad Shalit alietekwa nyara miaka minne iliyopita. Mwanasiasa huyo wa chama cha kiliberali cha FDP, ni waziri wa kwanza wa Ujerumani kutembelea Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2006.