Israel itaendelea na mazungumzo ya amani | Habari za Ulimwengu | DW | 08.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Israel itaendelea na mazungumzo ya amani

JERUSALEM:

Israel inataka kuendelea na majadiliano ya amani,licha ya mauaji yaliyotokea katika shule ya kidini ya Kiyahudi mjini Jerusalem.Msemaji wa serikali amenukuliwa akisema,Wapalestina wenye misimamo ya wastani wasiadhibiwe kwa sababu ya vitendo vya wafuasi wa itikadi kali.

Siku ya Alkhamisi,wanafunzi 8 wa Kiyahudi walifyatuliwa risasi na kuuawa na Mpalestina alieingia katika maktaba ya shule hiyo.Mshambulizi huyo baadae aliuliwa na mwanajeshi wa Kiisraeli.

Vikosi vya usalama vimewekwa katika hali ya tahadhari mjini Jerusalem,kufuatia mauaji hayo.Chama cha Hamas kimedai kuwa ndio kilichohusika na shambulizi hilo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com