Ispwisch: Mtu mwengine akamatwa katika kisa cha kuuawa makahama watano | Habari za Ulimwengu | DW | 20.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ispwisch: Mtu mwengine akamatwa katika kisa cha kuuawa makahama watano

Mtu wa pili ametiwa nguvuni kuhusika na mauaji ya makahaba watano katika mji wa Uingereza wa Ipswich. Haijafahamika iwapo mtu huyo ni mtuhumiwa wa kwanza au ni mshirika katika mauaji hayo. Mahakimu mjini Ipswich wameipa polisi siku moja zaidi kumhoji mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 37,ambaye ni mfanyakazi wa duka moja la vyakula, kabla ya kumfungulia mashitaka. Mtu wa pili aliyekamatwa , anasemekana anaishi katika eneo ambalo makahaba hao watano wakifanya shughuli zao. Maafisa wa upelelezi wanaendelea kutafuta taarifa zaidi mjini Ipswich na maeneo ya karibu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com