1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Watu tisa wameuwawa katika mzozo wa kikabila

23 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWj

Mzozo wa kikabila umesababisha vifo vya takriban watu tisa katika kijiji cha Zangari kilomita 60 kusini magharibi mwa mji wa Peshawar nchini Pakistan, watu wengine kumi na wawili wamejeruhiwa kwenye mzozo huo wakati wazee wa kijiji walipokuwa wakijaribu kuusuluhisha.

Chifu wa wilaya hiyo hata hivyo amesema hana hakika juu ya chanzo cha mzozo huo.